Rais John Magufuli amemtembelea Makamu wa Kwanza wa Zanzibar Maalim Seif, Serena Hotel.
Maalim Seif yuko hapo kwa mapumziko baada ya kutoka hostpitali ya Hindu Mandal, na amesema hali yake sasa inaimarika.
Kitendo cha Rais Magufuli kumtembelea na kumjulia hali kimepokelewa kwa hisia chanya na wananchi walio wengi, na inaonyesha mfano mzuri katika siasa za Tanzania.
KUNA JAMAA WANATEMBEA NA PIKIPIKI
WAKIONGOZANA KWA MBALI
UKIWA KWENYE FOLENI YA GARI
KAMA KIOO CHA GARI KIPO WAZI WANAKUTUPIA NYOKA WA PLASTIC
HASA KWA WASICHANA KISHA PIKIPIKI NYINGINE INATAKA KUKUSAIDIA KAMA
UMEYUMBA AU UMEGONGA AU UMEPATA UJASIRI NA KUSHUKA NDIO
WANACHUKUA KILA WANACHOKIWEZA
Hii imetokea gongo la mboto , buguruni , sinza na mbezi beach .mjulishe ndugu, rafiki yako asiache KIOO wazi !!!!
Sent as received
Wananchi tunataka kulitama bunge kupitia televisheni yetu ya taifa. Hatuoni sababu ya TBC kushindwa tena ukizingatia kwa sasa mfumo wa digitali unawezesha vyombo vya habari kuwa na channel zaidi ya moja bila gharama kubwa.
Namshauri waziri Nape Nauye aliengalie upya suala hili, ama pengine wana ajenda ya kufanya uongozi wa Rais wetu mpendwa Dk. Magufuli uonekane ni kandamizi na wenye kunyima raia wake haki ya kupata habari.
Ama hakika serikari ijiangalie upya kwenye hili suala. Ni mambo madogo kama haya yanatunyima sisi wananchi imani na serikali yetu.
Watu wengi hupata ajali barabaran kwa kutofata sheria na alama zilizowekwa pembezoni mwa barabara. Mwendo kasi uliopitiliza ni chanzo kimoja kinacho ongeza ajali nyingi barabarani. Tahadhari, zingatia sheria na funga mkanda kwa safari salama.
Zuia ukatili dhidi ya wanawake, Toa taarifa polisi kwenye dawati la jinsia.
Andika ujumbe wako hapa, hautajulikana lakini utakuwa umeshiriki kuokoa mamia ya wanawake wanaokumbwa na ukatili nchini.
Dondoo muhimu!
Ongeza au punguza kura ya bango kusisitiza ukweli au uhalisia wa jambo. Kumbuka kura yako ndio utawezesha ujumbe kutumwa kwa mamlaka husika ili kufanyiwa kazi.